Imefichuka: Kwanini Mourinho hakupata kibarua cha kuja Man United
Imeripotiwa kua Jose Mourinho alishindwa kupata kibarua cha
u-meneja Man United kutokana na kutopenda kulea wachezaji vijana.
Bosi huyo wa Chelsea yupo katika msukumo mkubwa katika msimu wake wa pili Chelsea kufuatia matokea mbaya ya kushangaza baada ya kupigwa 3-1 na Everton juzi jumamosi.
Mourinho alirejea tena kuifundisha Chelsea mwaka 2013 akitokea Real Madrid pamoja na kuhusishwa sana na Man United kufuatia kustaafu kwa Sir Alex Ferguson.
David Moyes ndiye aliyekipokea kijiti cha Fergie Old Trafford, lakini alidumu kwa miezi 10 pekee kabla ya ujio wa Louis van Gaal baada ya kombe la dunia mwaka jana.
Na kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza , Jose Mourinho ndie angefuatia baada ya Ferguson na alipitishwa lakini ilikuja kushindikana kutokana na kutopendelea kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi.
Kuleta wachezaji vijana na chipukizi kisha kuwakuza imekua ni sera ya Man United na imeshuhudiwa tangu kipindi cha miaka 26 ya Ferguson klabuni hapo.
Lakini kwa Mourinho yeye hupenda kuangalia uzoefu kwa wachezaji, ni sababu hiyo sasa kuna wachezaji 33 wa Chelsea wako nje ya klabu kwa mkopo.
Inadaiwa kua wawakilishi wa Man United walipokutana na kocha huyo walishindwa kushawishika kua angeweza kuendeleza sera yao ya kukuza wachezaji vijana.
Hata hivyo Mourinho alisisitiza kua aliikataa ofa ya Man United kwa ajili ya Chelsea, akisema "Nimekataa kila kazi duniani kwa ajili ya Chelsea. Bila shaka nilimwambia Sir Alex Ferguson ninataka kurejea Stamford Bridge."
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24
Imefichuka: Kwanini Mourinho hakupata kibarua cha kuja Man United
Reviewed by Steve
on
Monday, September 14, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 14, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment