Propellerads

Cech akizungumzia mechi ya jumamosi dhidi ya Chelsea



Petr Cech amesisitiza kua kazi yake kubwa na inayomhusu
yeye ni kuisaidia klabu yake ya Arsenal kupata point tatu muhimu na wala haina uhusiano na kucheza na klabu yake ya zamani.

Arsenal wanajiandaa kuumana na mahasimu wao wa jijini London, Chelsea jumamosi hii huku Mourinho akiwa na jukumu kubwa la kuhakikisha anashinda mchezo huo baada ya kua na mwanzo mgumu.

Cech ambaye aliichezea Chelsea kwa misimu 11 alijiunga na Gunners msimu huu baada ya kupoteza nafasi yake golini kwa Thibaut Courtois.

Na sasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Czech amewahakikishia mashabiki kua kazi yake ni kuhakikisha Gunners wanaibuka na ushindi Stamford bridge.

Mtandao wa Squawka umemnukuu mlinda mlango huyo akisema "Sijawahi kucheza Stamford Bridge kama mgeni kwa hiyo itakua ni experience mpya kwangu. Ninaenda sehemu ambayo ni kama familia yangu lakini kazi yangu kubwa ni kupata ushindi . Hivyo ndio inavyokua.

"Ukizingatia nimekaa muda mrefu sana pale. Najua kila kona ya uwanja , kwa hiyo kwangu hakutakua na kipya sana . Kipya kitakua ni kucheza dhidi ya Chelsea lakini ukianza kucheza swala kubwa ni kujiuliza kama utashinda?"

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24


Cech akizungumzia mechi ya jumamosi dhidi ya Chelsea Cech akizungumzia mechi ya jumamosi dhidi ya Chelsea Reviewed by Steve on Tuesday, September 15, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.