Propellerads

Busungu na matumaini makubwa kikosi cha Yanga



Straika mpya wa Yanga, Malimi Busungu ataendelea kupambana
hadi siku atakapopata nafasi ya kudumu.

Busungu amesema anajiamini, lakini anaamini uwezo wa wanaopata nafasi katika kikosi cha Yanga kwa sasa.

“Kweli kuna wachezaji wazuri pia ninalazimika kupambana kweli kupata namba. Lakini ninaamini nitaweza, ni suala la muda tu.

“Nataka kuitumia vizuri kila nafasi ninayopewa na mwalimu. Iko siku utaona tu,” alisema.

Mara nyingi, Busungu ambaye amejiunga na Yanga akitokea Mgambo Shooting amekuwa akiingia kipindi cha pili.


Wakati Kocha Hans van der Pluijm anaonekana kuwaamini zaidi washambuliaji wageni, Donald Ngoma kutoka Zimbabwe na Mrundi, Amissi Tambwe.
Busungu na matumaini makubwa kikosi cha Yanga Busungu na matumaini makubwa kikosi cha Yanga Reviewed by Steve on Friday, September 18, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.