Propellerads

Man United kukamilisha dili la Pedro wiki ijayo??!!




Manchester United wameripotiwa kupiga hatua kubwa katika kukamilisha
uhamisho wa nyota wa Barcelona, Pedro.

Baada ya wiki kadhaa za tetesi kuhusu hatma ya mhispania huyo, taarifa za sasa zinadai kua sasa Man United wanaweza kukamilisha usajili wao kwa nyota huyo.

Kwa mujibu wa gazeti la kihispania la Marca, mazungumzo baina ya vilabu hivyo viwili yanaendelea hivyo uhamisho unaweza kutangazwa rasmi mapema kabla ya Jumatano hii.

Hata hivyo ripoti nyingine kutoka hispania zinadai kua Pedro ambaye msimu uliopita hakupata nafasi sana kutoka na kuwepo combination ya kina Messi, Neymar na Suarez, ameombwa kuchezea Barcelona katika fainali ya UEFA Super Cup jumanne.

Man Utd wameanza vizuri EPL baada ya kuwafunga Tottenham 1-0 jana jumamosi.
Man United kukamilisha dili la Pedro wiki ijayo??!! Man United kukamilisha dili la Pedro wiki ijayo??!! Reviewed by Steve on Sunday, August 09, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.