Propellerads

Baada ya vipimo PSG, Di Maria anena ya moyoni




Angel Di Maria baada ya kusafiri kwa masaa 20 na kufika Qatar ambapo siku ya Jumanne
alifanyiwa vipimo vya afya, hatimaye amefaulu tayari kwa kujiunga na PSG inayoshiriki ligi ya Ufaransa.

Akiongea na BeIN Sports, Di Maria alisema maneno haya, “Nina furaha kwa kujiunga na PSG, ninachokijua ni kwamba PSG iliyoshinda makombe mengi kwenye msimu uliopita kule Ufaransa. Hiki ni kitu muhimu sana kwa club. Napia nataka kuvuka kihunzi ambacho ni robo fainali ya UEFA champions league pamoja na hii club. Naenda kujaribu kujitoa kadri niwezavyo kwenye huduma ya hii timu ili tufanikiwe. Tutajaribu kufika mbali kadri tunavyoweza ili tushinde ubingwa wa Ulaya”.

Di Maria ameweka wazi lengo lake na club hiyo ni kwamba kuchukua kombe la UEFA. Tuendelee kufuatilia mpango mzima utakavyoenda.
Baada ya vipimo PSG, Di Maria anena ya moyoni Baada ya vipimo PSG, Di Maria anena ya moyoni Reviewed by Steve on Thursday, August 06, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.