Jezi ya Di Maria imepata mrithi Man United, ni aliyeingia msimu huu!!
Nyota aliyesajiliwa na Man United msimu huu, Memphis Depay ameonesha
shauku yake ya kutaka kuvaa namba ya jezi iliyokua ikivaliwa na Di Maria, lakini anasubiri kwanza taratibu za uhamisho wa Muarjentina huyo zikamilike.
Depay anataka kutupia uzi huo bila kujali ugumu alioupata Di Maria katika jezi hiyo, kwani wengine huenda wakadhani ina 'gundu' , kwa sasa inadaiwa tayari ameshaongea na kocha Louis van Gaal kuhusu jezi hiyo
Vilabu vya Premier league vinatakiwa kuwasilisha majina ya wachezaji na namba zao mwisho Ijumaa hii lakini Man United bado hawajakamilisha zoezi hilo kutokana na ishu ya uhamisho wa Di Maria.
Depay ambaye anatumia jina la 'Memphis' katika jezi yake, anaweza kufanikiwa kuvaa jezi namba 7 mpaka kufikia Ijumaa kama mambo yakienda yalivyopangwa katika uhamisho wa Di Maria PSG.
Jezi ya Di Maria imepata mrithi Man United, ni aliyeingia msimu huu!!
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 06, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment