Arsenal kumsainisha Gonzalo Higuain
Arsenal wanadaiwa kutaka kumsajili nyota kutoka Napoli, Gonzalo Higuain baada ya
mkali huyo kukataa kuongeza mkataba mpya na klabu yake ya Serie A.
Mchezaji huyo ametuimia misimu miwili klabu hiyo ya Serie A, lakini jana jumanne wakala wake amethibitisha kua Higuain ametosa ofa ya kuongeza mkataba mpya.
Tangu zamani Higuain alihusishwa kutua Arsenal, ikiwa ni kabla hata hajajiunga Napoli mwaka 2013 akitokea Real Madrid.
The Gunners wanaonekana kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo, ambapo pia tayari wamehusishwa na nyota Karim Benema lakini hata hivyo dili hilo linaonekana kutoeleweka.
Higuain amefunga magoli 53 katika mechi 102 akiwa Napoli.
Arsenal kumsainisha Gonzalo Higuain
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 06, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment