Propellerads

Tetesi kubwa tano katika dirisha la usajili.





Ikiwa tayari dirisha la usajili likiwa limefunguliwa rasmi, leo tunamulika tetesi tano ambazo zinazungumzwa
sana na wengi kwa sasa.

SOMA: MAN UNITED KUMNASA MULLER

Sergio Ramos kujiunga Man United.
Nyota huyu wa Real Madrid amekua akihusishwa sana na kujiunga na Red Devils, japo bado haijaeleweka kama ni kweli yuko tayari kuhama. Huku suala hilo likibaki kua kizungumkuti, kuna baadhi ya ripoti zinadai kua ameomba kuondoka Real Madrid, huku wengine wakidai anataka kuendelea Hispania.


Paul Pogba kuelekea Barcelona au Real Madrid
Vilabu vingi vikubwa Ulaya vimeonesha nia ya kumnasa nyota huyu, lakini bado haijulikani ni wapi yeye anapotaka kutimkia, naa kama akiondoka Juve, inadsaiwa kua Barcelona wanataka kumsainisha huku Real Madrid nao wakionesha kuhitaji huduma yake.

Iker Casillas & Yohan Cabaye kuelekea Crystal Palace
Huku ikionekana kocha Alan Pardew akiimarisha kikosi chake kwa msimu ujao, inasemekana anaweza usajili wa nguvu kwa nyota wa PSG Yohan Cabaye na pia mkali mwingine kutoka Real Madrid, mkongwe Iker Casillas.

Zlatan Ibrahimovic kuingia English Premier League
ahi kucheza ligi kuu EPL lakini  anaweza kuja tena, kwani hali yake ya sasa PSG inaonekana kua mashakani . Tayari Ibrahimovic mwenyewe amekaririwa kutaka kuondoka, anahusishwa sana na vilabu vya Chelsea na Liverpool.

Juventus kuwanasa Isco na Oscar.
Bosi wa klabu hiyo ya kiitaliano, Massimo Allegri, karibuni alitaja nyota anaowawinda kuwasainisha, akasema anawahitaji Oscar kutoka Chelsea na Isco wa Real madrid. Hakuna mazungumzo rasmi mpaka sasa, huku Mourinho akidai bado anamhitaji Oscar kikosini.
Tetesi kubwa tano katika dirisha la usajili. Tetesi kubwa tano katika dirisha la usajili. Reviewed by Steve on Thursday, July 02, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.