Mourinho ataja timu mbili ngumu kwake.
Bosi wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, ameangazia msimu uliopita na kutaja timu mbili ambazo zilikua
ni mwiba mkali kwake.
SOMA: MESSI ATAJA TIMU MBILI ANAZOPENDA KUZIANGALIA
Bosi huyo mreno aliulizwa kua ni vilabu gani ambavyo vilimpa shida msimu uliopita, ambapo alitaja kwake kazi huipata anapokutana na Man City na Southampton.
"Ni lazima niwe mkweli na pia kutaja timu mbili, timu ambazo hatuwezi kuzifunga" aliiambia tovuti rasmi ya Chelsea.
"Manchester City mechi mbili na droo mbili, Southampton mechi mbili na draw mbili"
Mourinho alikua na msimu mzuri kipindi kilichopita, akichukua ubingwa kwa point nane zaidi.
Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid, amepata kuchukua mataji mengi katika kazi yake ya umeneja, ikiwemo taji la Serie A mara mbili, Champions League mara mbili, La Liga mara moja na EPL mara tatu.
Mourinho ataja timu mbili ngumu kwake.
Reviewed by Steve
on
Thursday, July 02, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, July 02, 2015
Rating:
