Propellerads

Headlines za usajili Ulaya leo.



Manchester United wataongeza dau lao la pauni milioni 30 kumtaka beki Sergio Ramos, 29, ikiwa tu Real Madrid nao
wataongeza dau kwa kipa David De Gea, 24 (Mirror) hata hivyo mama yake Ramos Paqui Garcia amesema mwanaye anataka kubakia Bernabeu (Antena 3).

Crystal Palace wanazungumza na Paris Saint-Germain kuhusu kumsajili kiungo Yohan Cabaye, 29 kwa pauni milioni 10 (Guardian).

Meneja wa Stoke City Mark Hughes atalipa pauni milioni 4.4 kumsajili kiungo kutoka Ghana Emmanuel Agyemang-Badu, 24 kutoka Udenese (Daily Star).

Manchester City watakabiliwa na ushindani mkali kuwapata viungo wanaowataka, Kevin De Bryne, 24 ambaye Wolfsburg wamesema hawatamuuza huku Paul Pogba wa Juventus akisubiri uchaguzi wa Barcelona (Daily Telegraph).

 City huenda wakaelekeza nguvu zao kwa kiungo wa Napoli Marek Hamsik, 27, kwa pauni milioni 20 (Sun).

Manchester City wanapanga kumchukua Pep Guardiola kuziba nafasi ya Manuel Pellegrini katika kipindi cha mwaka mmoja ujao, lakini Pellegrini amedhamiria kusalia Etihad na anataka kuanza mazungumzo ya mkataba mpya (Daily Star).

Aston Villa wanataka kumsajili Esteban Cambiasso, 34 baada ya mkataba wake kumalizika Leicester City (Sun). Newcastle United watalazimika kulipa pauni milioni 9 kama wanataka kumsajili mshambuliaji Bas Dost, 26 kutoka Wolfsburg (Daily Express). 

Beki wa Uruguay Sebastian Coates, 24, atahamia moja kwa moja Sunderland kutoka Liverpool (Guardian). Mshambuliaji wa Aston Villa Chrstian Benteke, 24 atakataa kuhamia Tottenham hata kama mkataba utafikiwa kwa sababu anataka kwenda Liverpool (London Evening Standard).

Kiungo wa Atletico Madrid Arda Turan, 28 anayenyatiwa na Chelsea na Manchester United atatangaza anakwenda wapi ifikapo Ijumaa (Manchester Evening News).

Chelsea wanatarajiwa kuthibitisha usajili wa mkopo wa Radamel Falcao, 29 baada ya kukubaliana maslahi binafsi na mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki (London Evening Standard).
Headlines za usajili Ulaya leo. Headlines za usajili Ulaya leo. Reviewed by Steve on Wednesday, July 01, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.