Luis Suarez: Premier League ndio bora zaidi ulimwenguni
Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Luis Suarez anaamini kua
English Premier League bado ni ligi ngumu na bora zaidi ulimwenguni.
Mchezaji huyo raia wa Uruguay aliondoka Liverpool kuelekea Nou Camp kwa dau kubwa tu msimu uliopita.
Nyota huyo anasema aliiaga ligi kubwa na bora zaidi ulimwenguni lakini pia hata kwa sasa anaamini yupo klabu bora zaidi.
"Sijisifii kama mchezaji bora zaidi duniani, lakini ni furaha yangu kucheza timu bora zaidi" aliiambia ESPN "EPL ni ligi bora zaidi ulimwenguni, lakini Barcelona ndio klabu bora zaidi."
"Bado tunahitaji magoli zaidi. Tunataka kua timu iliyoshinda mataji ya Champions league kwa mfululizo, tuna ari zaidi msimu huu. Tuko tayari kushinda"
Msimu uliopita Suarez aliwafungia Liverpool magoli 31.
Luis Suarez: Premier League ndio bora zaidi ulimwenguni
Reviewed by Steve
on
Friday, July 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, July 31, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment