Jerry Muro aondokewa na baba mzazi
Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amefiwa na
baba yake mzazi.
Babaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kulazwa kwa siku kadhaa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Akizungumza na mtandao mmoja nchini, Muro amesema msiba uko nyumbani kwa marehemu Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.
"Kama unavyojua kwa sisi Wakristo, kidogo taratibu zinakwenda kwa kusubiliana. Hivyo msiba ni pale Ubungo Maziwa nyumbani kwa marehemu," alisema Muro.
SALEHJEMBE INATOA POLE KWA JERRY NA WANAYANGA WENGINE.
MUNGU AMPUMZISHE MZEE MURO KWA AMANI.
Jerry Muro aondokewa na baba mzazi
Reviewed by Steve
on
Friday, July 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, July 31, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment