Propellerads

Kiiza adai mafanikio ya Yanga anahamishia Simba




Straika mpya wa Simba, Hamis Kiiza, amesema atahakikisha anaitumikia ipasavyo timu yake mpya na
kuipa mafanikio kama alivyofanya wakati anaichezea Yanga.

Kiiza amejiunga na Simba hivi karibuni na kupewa mkataba wa miaka miwili baada ya kuachwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili Desemba, mwaka jana.

 Kiiza amesisitiza atajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kuisaidia Simba ifikie malengo yake na atacheza kwa kiwango kikubwa kama alivyofanya awali.

“Nipo Simba na nawaahidi mashabiki wasiwe na wasiwasi juu ya kuisaidia timu hii kwenye suala zima la kupata mafanikio,” alisema Kiiza na kuongeza:


“Nitajitahidi kuhakikisha vile nilivyofanya nikiwa na Yanga navihamishia huku kwa sababu nimeondoka kule sikuwa na deni hata moja kwani mataji niliwapa.”
Kiiza adai mafanikio ya Yanga anahamishia Simba  Kiiza adai mafanikio ya Yanga anahamishia Simba Reviewed by Steve on Saturday, July 18, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.