Mechi ya Yanga na Gor Mahia, Cheki baadhi ya matukio katika picha
Yanga imepoteza kwa bao 2-1 katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Kagame.
Gor Mahia, mabingwa wa
Kenya ndiyo walioibuka na ushindi katika mchezo huo mtamu uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika kipindi cha kwanza.
Lakini Gor Mahia wakazidi kutamba katika kipindi cha pili kwa kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Michael Olunga.
Olunga aliyekuwa akiisumbua ngome ya Yanga tokea kipindi cha kwanza alifunga bao hilo baada ya kuwatoka Kelvin Yondani na Mbuyu Twite.
Yanga walitangulia kupata bao katika kipindi cha kwanza baada ya Gor Mahia kujifunga baada ya krosi ya Donald Ngoma, hiyo ilikuwa dakika ya 5.
Dakika ya 16, Shakava akasawazisha kwa kichwa baada ya Juma Abdul kumuangudha Walusimbi.
Dakika ya 24, Ngoma akalambwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.
Mwishoni mwa kipindi cha pili Yanga walicharuka na kushambulia mfululizo lakini haikuwazuia Gor kukomaa na kubakiza ushindi wao wa kwanza dhidi ya Yanga.
Mechi ya Yanga na Gor Mahia, Cheki baadhi ya matukio katika picha
Reviewed by Steve
on
Saturday, July 18, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, July 18, 2015
Rating:






