Frank Ribery: Sitamsemesha tena Boateng.
Winga wa Bayern Munich, Frank Ribery amesisitiza kua hatamsemesha tena mchezaji mwenzie klabuni hapo
, Jerome Boateng, kutokana na kutoheshimu imani yake ya dini ya kiislamu.
Ribery aliwaambia wachezaji wenzake kua waweke pombe mbali nae kutokana na misingi ya dini yake hairuhusu, aliwaambia wakati wakisherehekea ubingwa wa Bundesliga msimu uliopita.
Pamoja na ombi lake hilo, Boateng alichukua glasi kubwa ya pombe na kumvaa Ribery kisha akammiminia kichwani.
"Sitaongea na Boateng tena, alijua mimi ni muislam" alinukuliwa na gazeti la Daily mail.
Kwa upande mwingine, Golikipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer nae alionekana akimmwagia msichana mmoja pombe kichwani.
Frank Ribery: Sitamsemesha tena Boateng.
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 01, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, July 01, 2015
Rating:
