Propellerads

Yanga wazungumzia kuhusu hatma ya Kaseja.




Yanga imesema haina sababu zozote za kumzuia kipa Juma Kaseja kujiunga na timu nyingine kwa kuwa kweli haimhitaji.

Awali kulikuwa na taarifa kwamba Yanga inamfanyia Kaseja ntomanyongo kwa kushindwa kumuachia aende timu nyingine.


Lakini Mwanasheria wa Yanga, Frank Chacha amesema Kaseja yuko huru kujiunga na timu nyingine wakati kesi yao dhidi yake ikiendelea.

“Kaseja ameamua kuacha kazi mwenyewe, sasa si mwajiriwa wa Yanga na sisi tumefungua kesi. Si kweli hatutaki ajiunge na timu nyingine na wala hatuna sababu ya kumzuia.

“Kama atapata timu na kuna taratibu za kufanya, azifuate na kujiunga nayo. Sisi kesi yetu itaendelea mahakamani hadi hapo hukumu itakapotoka.

“Huenda kama tutashinda, basi akatulipa kupitia fedha anazolipwa. Hivyo ni vizuri kuliko kuendelea kukaa kijiweni kwa kuwa sisi tunamzuia,” alisema Chacha.


Kauli ya mwanasheria huyo imefuta utata kwamba Yanga ilikuwa ikimfanyia Kaseja ntimanyongo kwa kumzuia asisajiliwe na timu nyingine.
Yanga wazungumzia kuhusu hatma ya Kaseja. Yanga wazungumzia kuhusu hatma ya Kaseja. Reviewed by Steve on Saturday, June 20, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.