Unamjua mwafrika aliyepata kufunga fainali mbili za UEFA??......cheki hapa
Lionel Messi anaweza kua mchezaji pekee ambaye atakua amefunga katika mechi tatu za fainali za UEFA, lakini kuna
mchezaji wa kiafrika ambaye nae amepata kufunga katika michezo miwili ya fainali.
Kwa hizi takiwmu, Juve wataweza kweli kuwazuia Barcelona??!
Messi ni miongoni mwa wachezaji wanne ambao wamepata kufunga katika mechi mbili za fainali tokea kubadilishwa kwa mfumo wa mashindano na jina mwaka 1992, ambapo kabla mashindano haya yalijulikana kama European Champions Cup.
Mwaka 2009 katika fainali dhidi ya Manchester United, Messi ndiye aliyeifungia Barca goli la pili ambapo waliibuka washindi, na pia walipowachapa Man United 3-1 kwenye fainali mwaka 2011 Messi alifunga bao la pili pia kati ya matatu, hivyo ana magoli mawili ya fainali mpaka sasa.
Hata hivyo Messi alishindwa kwenye fainali dhidi ya Arsenal mwaka 2006, kwani hakuwemo kikosini.
Wachezaji wengine watatu kufunga magoli katika fainali mbili za UEFA ni Cristiano Ronaldo mwaka 2008 na 2014, Raul Gonzalez mwaka 2000 na 2002, na mwafrika pekee kwenye list hii ni Samuel Etoo mwaka 2006 na 2009.
Etoo alifunga bao la kusawazisha fainali dhidi ya Arsenal mwaka 2006 ambapo Barca walishinda 2-1, na pia katika fainali dhidi ya Man United mwaka 2009 ambapo alifunga goli la kwanza.
Kama ilivyo kwa Messi, Etoo ameshinda makombe matatu ya UEFA lakini alishindwa kuifungia timu yake dhidi ya Bayern Munich kwenye fainali ambayo walishinda 2-0.
Kiujumla Etoo amefunga mabao 30 katika mechi 78 za UEFA akiwa na vilabu vya Mallorca, Barca, Chelsea na Inter Millan, ambapo anaku mchezaji wa pili wa kiafrika kwa ufungaji baada ya Didier Drogba.
Unamjua mwafrika aliyepata kufunga fainali mbili za UEFA??......cheki hapa
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 06, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 06, 2015
Rating:
