Pique afunguka wanaompa shida wakiwa mazoezini.
Mlinzi wa FC Barcelona, Gerard Pique amefunguka kuhusu wachezaji wenzake ambao humpa wakati mbumu wakiwa
mazoezini.
Pique ambae aliingia Barcelona mwaka 2008 akitokea Manchester United, amekua ni beki wa kutumainiwa kwa sasa klabuni baada ya kustaafu kwa Carles Puyol.
Mkali huyo alisema kua ni kazi kumtaja mmoja pekee lakini wapo wengi wanaomuumiza kichwa.
"Ni vigumu kumtaja mmoja pekee, kazi ni ngumu hapa kila siku" aliiambia Daily Mail.
"Luis Suarez ana kipaji sana, Messi nadhani iko wazi, Haha Neymar nae yuko kwenye chati saivi. hao watatu wanatengeneza forward nzuri sana na wanatupa upinzani mkubwa mazoezini."
Pique kwa sasa anatoka na mwanamziki Shakira, na wana watoto wawili, Milan na Sasha. Mkali huyu ana elimu ya kutosha kwani ana post-graduate ya Economics kutoka ESE Bussines school.
Pique afunguka wanaompa shida wakiwa mazoezini.
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 06, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 06, 2015
Rating:
