Propellerads

Transfer Updates: Nyota watano wanaotizamiwa kuondoka Man United.




Huku habari ya usajili na tetesi zake zikitawala vyombo mbali mbali vya habari kwa sasa, leo nakuletea orodha
ya nyota watano ambao wanatizamiwa na kupewa nafasi kubwa kuondoka klabuni Old Trafford.

Robin Van Persie
Mdachi huyu siku za hivi karibuni ameripotiwa kudai kua anataka kucheza kikosi cha kwanza katika kila mechi, lakini bado haijaeleweka kama anaweza kupata nafasi hiyo Old Trafford. Akiwa na miaka 31 kwa sasa, tayari amehusishwa na vilabu kadhaa vya Serie A vilevile hata klabu kutoka Uturuki, Galatasaray, huku ripoti nyingine zikidai kua kuondoka kwake kutakua ni sehemu ya dili la kumleta Nicolas Otamendi kutoka Valencia, kuja Man United.

Angel Di Maria
Japo aliwahi kukaririwa siku za hivi karibuni kua atabakia Man United, lakini bado hakuna uhakika kama kweli atabaki au ataondoka klabuni, tayari Paris Saint Germain na Bayern Munich wameonesha nia ya kumpata mkali huyo.

Rafael
Kocha Louis van Gaal anadaiwa sio shabiki saana wa nyota huyu ambae msimu uliopita alitawaliwa na majeraha, huku huku nafasi yake kama beki wa kulia ikibakia dhaifu. Hata ivyo hali ya sasa inaonekana anaweza kuoneshwa mlango wa kutokea kwani Man United wanadaiwa kutaka kutafuta beki mwingine wa kulia.

Javier Hernandez
Mkali huyu atarejea kutokea Real Madrid alikokua akichezea kwa mkopo, ambapo Los Blancos hawaonesha nia ya kumnunua baada ya mkopo kuisha. Hata hivyo Man United nao hawajaonesha kuvutiwa sana kwa sasa na mkali huyo ambae Inter wanadaiwa kuonesha nia ya kumnasa.

David De Gea
Mhispania huyo ni kama imebaki kidogo tu awe wa Real madrid kabisa, kwani yamebaki makubaliano tu katika upande wa bei, ambapo Real wanadaiwa kutaka kutoa kiasi cha pauni mil. 30.
Transfer Updates: Nyota watano wanaotizamiwa kuondoka Man United. Transfer Updates: Nyota watano wanaotizamiwa kuondoka Man United. Reviewed by Steve on Friday, June 19, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.