Propellerads

Tajiri mwafrika kuwania kuinunua Arsenal.




Mtu tajiri zaidi Afrika na bilionea kutoka Nigeria, Aliko Dangote yuko katika harakati za kutaka
kuinunua klabu ya Arsenal.

Dangote ambaye anashikilia nafasi ya 67 duniani kwa ukwasi, anawazidi hata wamiliki wa sasa wa klabu hiyo ambao ni Stan Kroenke ( anamiliki 66.64 % ) na Alisher Usmanov ( asilimia 29.11 % ).

Mnaijeria huyo ambae si mara ya kwanza kutaka kutaka kuinunua Arsenal baada ya mwaka 2010 kukataliwa mpango wake, lakini inasemekana anajiandaa kuwania tena.

"Tulikua wengi tuliotaka kufanya kununua 2010, na tulifikiria kuhusu bei , ila waliokua wanataka kuiuza waliweka kiwango kikubwa sana" aliiambia BBC Hausa.

"Tulishindwa, kwa kua tulikua tunafanya vitu vingine pia, hasa kuendeleza viwanda vyetu."

Dangote hata hivyo ameikosoa Arsenal na kocha wake Arsene Wenger nakushauri kua wanatakiwa wabadilike ili waweze kupata mafanikio makubwa.

" Wanafanya vizuri, lakini wanahitaji mipango mingine" aliongeza.

"Wanahitaji mwongozo mwingine kuliko hali ya sasa, ambapo wanatengeneza tu wachezaji na kuwauza"
Tajiri mwafrika kuwania kuinunua Arsenal. Tajiri mwafrika kuwania kuinunua Arsenal. Reviewed by Steve on Thursday, June 18, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.