Stars yapata kipigo cha aibu tena.
Matumaini ya Taifa Stars kushiriki michuano ya Chan yametoweka baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa kufungwa na Uganda kwa mabao 3-0.
Stars imepoteza mchezo huo leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar baada ya kuchapwa na wageni wake Uganda.
Wakati leo imepoteza, inasubiri kusafiri kwenda Uganda kuwavaa The Cranes, jambo ambalo linasubiri miujiza au aibu zaidi.
Wakati Stars imepoteza mechi hiyo, Kocha wake mkuu, Mart Nooij alitoka uwanjani hapo kama kiongozi wa serikali baada ya kusindikizwa na askari pamoja na mtu mmoja mwenye umbo kubwa anayeaminika ni mfanyakazi wa TFF.
Nooij amekuwa akipigiwa kelele na Watanzania ambao wanaonekana wamechoka na kufungwa kila kukicha.
Mholanzi huyo anaonekana wazi kuishindwa kazi yake, lakini TFF imekuwa inasita kumuondoa.
Hata hivyo, Watanzania wamekuwa wakipiga kelele kuhusiana na Mshauri wa Ufundi wa Rais wa TFF aitwaye Peregrinus Rutayuga ambaye anaonekana pia kuwa tatizo.
Wadau wamekuwa wakipiga kelele, Nooij, Rutayuga na memba wengine wa benchi hilo watupiwe virago.
Stars yapata kipigo cha aibu tena.
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 21, 2015
Rating:
