Stars waendelea na mazoezi, waandishi marufuku!!
Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea na mazoezi leo kujiandaa kwa ajili ya kuivaa Misri Juni 14.
Stars imefanya mazoezi leo lakini
leo saa 11 jioni ina safari ya kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya kambi.
Stars itaweka kambi nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Misri kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Kocha Mart Nooij ndiye aliongoza kikosi hicho katika mazoezi ya leo licha ya kuwa waandishi walizuiwa kuingia.
Mtandao mmoja maarufu umeripoti kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakizuiwa na uongozi wa Gymkhana kwa madai si wanachama wa klabu hiyo.
Hata hivyo wamekuwa wakiomba
kupewa ruhusa angalau ya kufanya kazi yao kwa kushuhudia mazoezi ya
Stars tu kwa takribani saa mbili, halafu waondoke, lakini imekataliwa
kabisa.
Haijajulikana kwa nini hali hiyo
inatokea wakati Gymkhana wamekuwa wakiawaalika waandishi katika michuano
mbalimbali inayofanyika klabuni hapo.
Askari waliendelea kusisitiza kuwa waandishi hawaruhusiwi kuingia na TFF wanalijua suala hilo.
Stars waendelea na mazoezi, waandishi marufuku!!
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 04, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 04, 2015
Rating:
