Propellerads

Messi ataja wachezaji watatu ambao huogopa kukabiliana nao....na Ronaldo yumo??!!, soma hapa



Mkali kutoka anayekipiga katika klabu ya Barcelona, Lionel Messi ametaja wachezaji watatu hatari kwake huku hasimu wake mkubwa
Cristiano Ronaldo akiwa ni miongoni mwao.

Alianza kwa kutaja wachezaji wenzie klabuni Nou Camp ambao hukabiliana nao kila siku katika mazoezi, kisha akataja na wakali kutoka vilabu vingine.

Nyota huyo kabla aliulizwa kwanza ni upinzani gani mkali ambao hua anakutana nao, akasema ni swali gumu sana kwake.

"Woow, hiyo ni ngumu sana!!" aliiambia Squawka

"Sitaki kutajahata mmoja, lakini nina furaha kua wengi wao wanachezea Barcelona na pia nimepambana nao katika timu za taifa"

"Nimepambana na Neymar, Iniesta,na Xavi ni wakali sana, pia bila shaka kuna Cristiano, Robben na Ribery. Lakini siwezi kutaja mmoja pekee."

Soma: Unawajua mabeki ngangari wa Suarez!!

Uhasimu wa Messi na Ronaldo umeanza mbali kidogo, huku Ribbery na Roben walikumbana na Messi katika nusu fainali ya UEFA ambapo Bayen Munich walishinda kwa jumla ya magoli 7.

Messi ataja wachezaji watatu ambao huogopa kukabiliana nao....na Ronaldo yumo??!!, soma hapa Messi ataja wachezaji watatu ambao huogopa kukabiliana nao....na Ronaldo yumo??!!, soma hapa Reviewed by Steve on Thursday, June 04, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.