Propellerads

Simba wako hatua za mwisho kumnasa beki mrundi.


Kamati ya Usajili ya Simba iko katika hatua ya mwisho kumsajili beki wa pembeni, Nimubona Emiry ambaye ni kiboko.

Emiry ana uwezo wa kucheza kwa ustadi mkubwa beki zote mbili za kulia na kushoto ambazo Simba zaidi wanawategemea Ramadhani Kessy na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.


Emiry raia wa Burundi bado yuko Vital’O ya Burundi na tayari Simba imeanza mazungumzo naye ambayo yamefika katika nzuri.




Iwapo watakubaliana, kiongozi mmoja wa Simba anaweza kukwea pipa na kwenda kumsajili beki huyo anayeaminika ataleta upinzani mkubwa kwa mabeki wa pembeni wa Simba.
Simba wako hatua za mwisho kumnasa beki mrundi. Simba wako hatua za mwisho kumnasa beki mrundi. Reviewed by Steve on Saturday, June 13, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.