Propellerads

Schweinsteiger kujiunga Man United.




Lengo la Manchester United kumnasa mkali Bastian Schweinsteiger linaweza kutimia, kwani mkali huyo anaweza
kuondoka Bayern Munich kwa mujibu wa mkongwe wa soka Ujerumani, Lothar Matthaus.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani amekuwepo kwa kipindi cha miaka 13 Bayern, huku akipata mafanikio makubwa, lakini mkataba wake wa sasa unatarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu ujao.

Mkongwe Matthaus anaamini hii itakua ni nafasi nzuri kwa Schweinsteiger kuangalia maisha mengine tofauti, akiamini kua Manchester United itakua sehemu nzuri na sahihi kwa mkali huyo.

"Katika hatua hii ya mwisho katika career yake, Schweinsteiger anahitaji kocha atakayemuamini na kumtengenezea mfumo" Matthaus aliandika katika makala yake Sport Bild.

"Kama Schweinsteiger atapata ofa kutoka klabu yeyote kubwa Ulaya,nitamshauri ahame majira ya kiangazi"

"Kama hizi tetesi ni za kweli, kua Louis van Gaal anamhitaji Manchester United, Schweinsteiger anatakiwa kulifikiria hili kwa umakini.

"Kama Van Gaal anamhitaji, atamchezesha pale ambapo anapaweza"

Kiungo huyo amekua akisumbuliwa na majeraha siku za hivi karibuni, lakini hali hiyo haijamzuia kuisaidia Bayern Munich kuchukua ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya tatu mfululizo.
Schweinsteiger kujiunga Man United. Schweinsteiger kujiunga Man United. Reviewed by Steve on Friday, June 19, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.