Rooney amtaja nyota wa EPL anaetaka awepo Man United.
Nahodha wa klabu ya 'mashetani wekundu' Man United, amemtaja nyota chipukizi ambae angependa awepo
kikosini Old Traford.
Rooney amefunguka kua, angependa kumuona fowadi wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane akiwa kikosini Man United, ambapo hata hivyo Man U wamedaiwa kuonesha nia ya kumhitaji.
"Ametisha uwanjani msimu huu" aliiambia ESPN.
"Amefanya makubwa, ni mchezaji chipukizi Uingereza, itapendeza sana nikiwa nae katika kikosi changu"
Kane, mwenye umri wa miaka 21 kwa sasa, msimu uliopita aliifungia Tottenham magoli 31 katika mechi 51 na kutoa usaidizi zaidi ya mara sita kwa wenzake.
Japokua Man United wameonesha nia ya kumuhitaji, inadaiwa kua bado Tottenham hawana mpango wa kumuuza chipukizi wao huyo mwenye kipaji kikubwa.
Rooney amtaja nyota wa EPL anaetaka awepo Man United.
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 18, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 18, 2015
Rating:
