Petr Cech kuchukua vipimo vya afya leo.
Mlinda mlango anatarajiwa kuchukua vipimo vya afya leo klabuni Arsenal, huku kukija baada ya kuripotiwa
uhamisho wa thamani ya pauni mil 10.9 akitokea Chelsea.
Wapinzani hao wa Premier League wanaripotiwa kukubaliana dili kwa mkongwe huyo wa Chelsea ambaye kukamilika kwa mpango huu kutahitimisha safari yake ya miaka 11 Old Traford.
Cech ambaye msimu uliopita alicheza kama kipa chaguo la pili baada ya Thibaut Courtois, uhamisho wake waweza kukamilika muda wowote karibuni.
BBC Sport wamedai kua mambo ya mwisho yanafanyika kumaliza swala hili, leo anafanyiwa vipimo vya afya amabayo ni hatua ya mwisho kukamilika kwa dili.
Mlinda mlango wa zamani wa The Gunners, Bob Wilson, anaamini kua usajili wa mkali huyu utaifanya Arsenal kufanya vizuri zaidi msimu ujao.
Petr Cech kuchukua vipimo vya afya leo.
Reviewed by Steve
on
Friday, June 26, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, June 26, 2015
Rating:
