Kocha mpya wa Simba atua leo Dar.
Kocha mpya wa Simba, Dylan Kerr amewasili jijini Dar es Salaam amesema atapambana kuhakikisha
Simba inafanya vema.
Kerr raia wa Uingereza amewasili jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Simba, Collins Frisch.
“Sijui vitu vingi kuhusiana na soka la Tanzania lakini lengo ni kutengeneza kikosi bora chenye kuleta ushindi.
“Kwa sasa inaweza kuwa mapema sana kuzungumzia mambo mengi, lakini najua tutafanikiwa tukishirikiana.
“Simba ni timu kubwa na maarufu, hivyo ushirikiano utakuwa nguzo ya kufikia mafanikio,” alisema.
Kocha huyo anachukua nafasi ya Goran Kopunovic raia wa Serbia ambaye Simba iliamua kuachana naye baada ya kutaka Sh milioni 100 ili asaini mkataba wa miaka miwili.
Kocha mpya wa Simba atua leo Dar.
Reviewed by Steve
on
Friday, June 26, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, June 26, 2015
Rating:

