Propellerads

Neymar aiwezesha Brazil kuanza vyema.



Timu ya taifa ya Brazil imeanza vyema michuano ya mataifa ya America kusini (Copa America) baada ya kuibuka na ushindi wa
magoli 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Peru katika mechi ya ufunguzi ya kundi C iliyopigwa nchini Chile usiku wa kuamkia leo.





Mapema dakika ya 3′ Peru waliandika goli la kuongoza kupitia kwa Christian Cueva, lakini dakika mbili baadaye, mshambuliaji wa Barcelona, Neymar akaisawazishia Brazil goli hilo.

Dakika ya 90′ ya mchezo Douglas Costa alipachika goli la pili na la ushindi kwa vijana wa Brazil (Samba boys).

Hata hivyo, Brazil walihangaishwa na Peru na wakasubiri dakika za jioni kabisa kufunga goli la ushindi.
Katika mchezo mwingine Colombia walishindwa kutamba mbele ya Venezuela baada ya kuchapwa 1-0
Neymar aiwezesha Brazil kuanza vyema. Neymar aiwezesha Brazil kuanza vyema. Reviewed by Steve on Monday, June 15, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.