Cheki picha mchezaji wa EPL apiga gambe mpaka 'kusizi'.
Huu ni wakati wa likizo kwa wachezaji wa timu za ulaya na kwingingine duniani. Wakiwa kwenye ligi kawaida huwa hawapati
muda wa kujiachia kufanya mambo ya starehe sana hasa kulewa kupindukia.
Sasa muda wa likizo ndio muda wa fungulia mbwa, mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish amepigwa picha na mtu asiyejulikana akiwa chini hoi baada ya kupiga gambe. Grealish ambae ana miaka 19 habari zake pamoja na picha zimesambaa sana mtandaoni na inasemekana kwamba clun hiyo itakutana nae hivi karibuni kutokana na picha hizo.
Uongozi wa Villa umesema kwamba wanajua kwamba picha za mchezaji wao zinasambaa sana na washamuita kuwa na kikao nae. Kuhusu maamuzi ya kinidhamu yatabaki kuwa mambo ya ndani ya club hiyo.
Lakini baada ya muda w akusambaa hizo picha, Jack Greaish alitumia account yake ya twitter kwa kukanusha kwamba sio yeye kwenye picha.
Cheki picha mchezaji wa EPL apiga gambe mpaka 'kusizi'.
Reviewed by Steve
on
Monday, June 15, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, June 15, 2015
Rating:




