Propellerads

Mourinho kumtengea pauni mil. 15 mghana huyu.




Bosi wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, anadaiwa kutenga kiasi cha pauni mil. 15, kuifukuzia saini ya chipukizi kutoka
Ghana, Abdul Baba Rahman.

Mchezaji huyo anayecheza beki ya kushoto uwanjani, aling'aa na Augsburg inayokipiga Bundesliga, na kama akitua Chelsea ataziba nafasi ya Fillipe Louis ambaye anadaiwa kutaka kurejea Atletico Madrid.

Luis ambaye alijiunga The Blues kwa dau la pauni mil. 16 akitokea Rojiblancos (Atletico Madrid) msimu uliopita, ameshindwa kuonesha makali ya kutosha beki ya kushoto hali iliyopelekea Mourinho kumchezesha zaidi Cesar Azpilicueta katika nafasi hiyo.

Baba Rahman anaweza kufuata nyayo za mghana mwenzie, Michael Essien , kwa sasa ana miaka 20, akiwa ameichezea Augsburg mechi 31 msimu uliopita na kutoa usaidizi katika magoli matano.

Alianza kuonenakana katika kikosi cha Ghana 'Black Stars' Septemba 2014, na alikuemo kwenye kikosi cha Ghana kilichoshiriki African Cup of nations 2015.
Mourinho kumtengea pauni mil. 15 mghana huyu. Mourinho kumtengea pauni mil. 15 mghana huyu. Reviewed by Steve on Thursday, June 18, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.