Mchezaji mmoja afunguka kinachowakimbiza Mbeya City.
Imefahamika kuwa maslahi madogo yaliyopo kwenye Klabu ya Mbeya City ndiyo sababu kubwa ya wachezaji nyota
kuikimbia timu hiyo.
Mbeya City ambayo imekuwa na jina kubwa ndani ya misimu miwili iliyocheza Ligi Kuu Bara, imekimbiwa na wachezaji wanne waliokuwa katika kikosi cha kwanza ambao ni Peter Mwalyanzi aliyetua Simba, Deus Kaseke (Yanga), Paul Nonga na Anthony Matogolo (Mwadui FC).
Mtandao mmoja maarufu umemkariri Nonga ambaye ametua Mwadui na kupewa mkataba wa mwaka mmoja, akisema kilichomuondoa ni maslahi na hakuwa na jinsi.
“Mwadui wamenipa dau zuri zaidi ya lile la Mbeya City. Mpira ndiyo kazi yangu, hivyo naangalia maslahi na si kingine,” alisema Nonga.
Ikumbukwe kuwa dirisha la usajili bado halijafunguliwa na kuna uwezekano wa wachezaji zaidi kuihama timu hiyo ambayo nayo imewasajili Gideon Brown aliyetokea Ndanda, Haruna Shamte (JKT Ruvu) na Joseph Mahundi (Coastal Union).
Mchezaji mmoja afunguka kinachowakimbiza Mbeya City.
Reviewed by Steve
on
Friday, June 05, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, June 05, 2015
Rating:
