Mambo matano usiyoyafahamu kuhusu Pogba.
1) Wazazi wake ni mchanganyiko wa Guinea na Congo, ana wadogo wadogo wawili Mathias na Florentin ambao nao ni wanasoka pia japo hawana mafanikio kama Pogba. Mathias anachezea Crewe Alexandra kama forward huku Florentin anaichezea Saint-Etienne.
2) Wakati Manchester walipomleta aje England akitokea
Le Havre, wafaransa hao waliwatuhumu Man United kwa kuwaibia kipaji chao chipukizi. Rais wa Le Havre alidai ku Man United walimlipa Pogba puni 87 000 na kumnunulia nyumba, hata hivyo FIFA walyachunguza malalamiko hayo na mwishoe Man United hawakuonekana na hatia yoyote.
3) Pogba aliichezea Man United kuanzia 2009 mpaka 20012 alipoondoka akiwa mchezaji huru, kwani hakusaini mkataba mwingine. Hii ilimkasirisha kocha Sir Alex Ferguson ambae aliibuka na kudai Pogba alikua na kiburi na hakua mtiifu, Pogba naye baadae akajibu madai hayo kua Ferguson hakua akimruhusu kucheza na alipoomba kuondoka akakasirika.
4)
jina la utani kutoka kwa mashabiki wake ni " II Polpo Paul" ambalo humaanisha "Pweza Paul" kutokana na urefu wa miguu yake. Ana urefu wa futi 6'2 huku asilimia kubwa ya urefu wake ikiwa ni miguuni, hivyo mashabiki wanafananisha na miguu ya pweza.
5)
Mwaka 2013 Pogba alipewa tuzo ya 'Golden Boy' kama mchezaji bora Ulaya chini ya miaka 21. Aliiwakilisha Ufaransa katika level zote ambapo alikua nahodha kikosini mwaka 2013 walipochukua kombe la dunia kwa wachezaji chini ya miaka 20 ambapo alichukua uchezaji bora wa michuano, pia huko Brazil kombe la dunia mwaka 2014 alichukua tuzo kama mchezaji bora chipukizi.
Mambo matano usiyoyafahamu kuhusu Pogba.
Reviewed by Steve
on
Tuesday, June 16, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, June 16, 2015
Rating:
