Kocha bora afrika mashariki asema haya kuhusu kuinoa Simba.....soma hapa
Akizungumza na mtandao mmoja maarufu kutoka Brussels nchini Ubelgiji, Amrouche mwenye asili ya Algeria amesema hajawahi kuwania kuinoa Simba.
"Nimesikia kutoka kwa rafiki yangu kwamba nawania kuifundisha Simba, si kweli.
"Inawezekana wao wangependa iwe hivyo, ila ndoto yangu ni kufanya vizuri katika michuano ya Afrika nikiwa na timu ya taifa.
"Ingekuwa timu ya taifa ya Tanzania, sawa lakini klabu, niwe mkweli si ndoto yangu," alisema Kocha huyo bora wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Amrouche alibeba tuzo ya kocha bora Afrika Mashariki na Kati baada ya kuiwezesha Kenya iliyokuwa na kikosi dhaifu, kubeba ubingwa wa Cecafa.
Pia Amrouche amekuwa mmoja wa makocha waliokifanya kikosi cha timu ya taifa ya Burundi kuwa moto.
Kabla ya kuifundisha Burundi, aliwahi kuwa kocha wa DC Motema Pembe ya DR Congo na kuiwezesha kubeba mataji lukuki.
Hivi karibuni, vyombo vya habari viliripoti kwamba Amrouche alikuwa kati ya makocha wanaowania kuinoa Simba.
Hata hivyo, uongozi wa Simba, bado haujatangaza kocha yupi ambaye unapambana ili kumpata baada ya zaidi ya makocha watano kuomba nafasi ya kuinoa.
Kocha bora afrika mashariki asema haya kuhusu kuinoa Simba.....soma hapa
Reviewed by Steve
on
Monday, June 01, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, June 01, 2015
Rating:

