Propellerads

Bale anataka kucheza nafasi ya Ronaldo.




Mkali Gareth Bale anadaiwa kutaka kucheza upande ambao huchezwa pia na mshindi wa
Ballon d'Or Cristiano Ronaldo msimu ujao.

Man United kuvunja rekodi kwa Bale??

Kulingana na vyombo vya habari vya Hispania, Bale amekutana na mabosi wa Los Blancos kuzungumzia hatma yake klabuni hapo, lakini pia aliomba kucheza winga ya kushoto msimu ujao, nafasi  ambayo Ronaldo hucheza.

Bale aliuambia uongozi wa klabu kua hajisikii vizuri anapocheza winga ya kulia labda ndio sababu haoneshi makali yake, japokua ndio nafasi anayocheza tangu atue klabuni hapo. Habari hii inaweza isiwe nzuri kwa Cristiano Ronaldo.

Hata hivyo kumekuwapo na uvumi kua msimu ujao Ronaldo anaweza kuchezeshwa kama mshambuliaji wa kati, lakini Ronaldo mwenyewe anaonekana kufurahia kucheza kushoto kwani anakua huru kufanya lolote na hata kuingia ghafla akitaka.

Wakala wa Bale, Jonathan Barnett amedaiwa kuusisitiza uongozi wa Real madrid kua anataka kuona mchezaji wake nae anataka kuchukua Ball on d'or hivyo Madrid wanatakiwa kumweka katika kiwango chake, Los Blancos wanaweza kufanya hivyo kwani hawajaonesha nia ya kumwachia Bale.




Bale anataka kucheza nafasi ya Ronaldo. Bale anataka kucheza nafasi ya Ronaldo. Reviewed by Steve on Friday, June 05, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.