Propellerads

Simba, Yanga kwa hili wako pamoja

Uongozi wa Simba umesema uko tayari kukaa meza moja na watani wao Yanga ili kulijadili suala la malipo ya haki za runinga kutoka
Azam Media Group.
Salehjembe amemkariri mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe akisema wako tayari kukutana na kila timu inayoshiriki Ligi Kuu ikiwemo Yanga.
Hans pope


“Hili suala halikuwa sahihi, tunahitaji kukaa na kulijadili. Hata wakiwa Yanga sawa, pia timu nyingine zinazoshiriki ligi.
“Itakuwa vizuri sana kama tutakutana wote yaani timu zinazoshiriki ligi, pia TFF na hao wadhamini.
“Kwangu naamini Simba na Yanga zilistahili kupata zaidi ya fedha hizi zilizotolewa,” alisema Hans Poppe.
Alipoulizwa kuhusiana na Simba kuwahi kusaini mkataba huo bila ya kufanya uchunguzi, alisema haya.
“Alikwenda kusaini harakaharaka alikuwa Rage, alikuwa na kawaida ya kutokaa na kamati yake ya utendaji na kujadili.
“Amekwenda amesaini na sasa hili ni tatizo. Sisi tungependa kulimaliza hili kwa uzuri kabisa,” alisema Hans Poppe.
Simba, Yanga kwa hili wako pamoja Simba, Yanga kwa hili wako pamoja Reviewed by Steve on Wednesday, May 20, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.