Propellerads

Nini kinafuata kwa Di Maria?

Angel Di Maria hajakua katika kiwango chake Old Traford hadi kupelekea kuwepo matazamio ya yeye kutimkia Paris Saint German au Bayern Munich, lakini yote kwa yote nini kinafuata
kwake??

                                                 


Mchezaji huyo mwenye miaka 27 aliingia Man U kwa ada ya pauni mil. 59.7 akitokea Real madrid mwanzoni kabisa mwa msimu huu, lakini ameshindwa kufikia matarajio ya wengi pale Old Traford.

Aliyaanza vizuri tu maisha yake pale Man U, kwani mechi tano za mwanzo alifunga magoli matatu na kutoa usaidizi mara tatu pia-lakini alishindwa kabisa kudumu kwenye hicho kiwango.

Kwa usajili uliokua rekodi kubwa pale EPL huku matazamio yakiwa kufikia malengo ya Van Gaal kumaliza nafasi nne za juu-top four . lakini baada ya kua chini ya kiwango kunatia mashaka kuhusu future ya Di Maria klabuni hapo.

Katika mechi 21 zilizopita za Man U ambazo Di Maria alicheza hakufanikiwa kucheka na nyavu walau hata mara moja.

PSG na Bayern Munich wameonesha nia ya kusainisha mkali huyo, lakini bado haijafahamika kama Van Gaal anaweza kumruhusu kuondoka baada ya msimu huu pekee aliochezea Man U.

Juan Mata na Ashley Young wameonekana kucheza nafasi yake mara kadhaa, lakini sio tiketi ya kusema Man U watamuuza japo kaonesha kiwango cha chini.

Msimu huu akiwa Di Maria amecheza Michezo 31, akifunga magoli manne pekee na kutoa usaidizi mara 12.
Nini kinafuata kwa Di Maria? Nini kinafuata kwa Di Maria? Reviewed by Steve on Wednesday, May 20, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.