Propellerads

Licha ya rekodi ya ufungaji, magoli ya Ronaldo hayana maana??

Ronaldo amepata kuifungia Real Madrid mabao kibao na kuvunja rekodi nyingi huku akiwa na taji
moja tu la La Liga katika misimu sita aliyo icheza Los Blancos.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ureno amejipatia umaarufu wa kua miongoni mwa wafungaji hatari wa muda wote, lakini rekodi zake za ufungaji pamoja na kumletea mafanikio makubwa yeye, hazijaipa mafanikio makubwa klabu yake.

                                       



Ronaldo amekuepo Real Madrid kwa misimu sita, akifungia magoli 222 katika michezo 199 ya ligi ukiwa ni wastani wa magoli 37 kwa kila msimu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Man United tangu aingie ligi ya Hispania , Messi amepata kua mfungaji bora mara tatu katika misimu hii sita ya Ronaldo, ambapo ufungaji huu wa Messi umeiwezesha Barca kuckukua mataji manne ya La liga ndani ya kipindi hicho.

Japo hua kuna ubishani unaoendelea miongoni mwa mashabiki wa soka kua kati ya Messi na Ronaldo nani zaidi, ukweli ni kua Messi ameiwezesha Barca kuchukua taji La Liga mara 7 ndani ya misimu 11, huku Ronaldo akiwawezesha Madrid kuchukua ubingwa mara moja ndani ya misimu sita.
Licha ya rekodi ya ufungaji, magoli ya Ronaldo hayana maana?? Licha ya rekodi ya ufungaji, magoli ya Ronaldo hayana maana?? Reviewed by Steve on Wednesday, May 20, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.