Mazungumzo ya usajili Manchester United
Manchester United wamehusishwa katika kutaka kupata saini za akina Muller, Mats Hummels, Bastian Schwensteiger, Otamendi na Raheem Sterling, ripoti
zinadai!
Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc ameliambia chapisho la Ujerumani Kicker kua Hummels hataondoka klabuni.
Imeripotiwa Man U walitenga dau la Pauni mil. 40 kwa ajili ya mjerumani huyo, ambaye hata hivyo hajaonesha nia ya kutaka kuondoka klabuni kwake.
Kicker pia wanadai Old Traford wanaiwinda saini ya Mchezaji wa Bayern Schwernsteiger ambaye mkataba wake wa sasa klabuni hapo utaisha mwaka 2016 ambapo labda anaweza kua rahisi zaidi.
Pia inaripotiwa kua Van gaal ameonesha kumtaka Muller ambaye alikua mchezaji wake kikosi cha kwanza kipindi anafundisha Bayern Munich, Muller ameonekana kutokua na mahusiano mazuri na kocha wake wa sasa Pep Guardiola, lakini itawalazimu Man U kutoa kiasi cha pauni mil 40 au zaidi ili kumnasa mchezaji huyo.
Pia huko klabuni Valencia, uongozi wa klabu hiyo umesema hautamwachia mchezaji wao Odamenti kama Man U hawataoa dau chini ya pauni mil 50. Odamenti alidaiwa kua na mazungumzo binafsi na Man U.
Mchezaji wa mwisho kuhusishwa na Man U, ni mkali anayetaka kuikimbia Liverpool, Raheem Sterling, kama ESPN wanavyodai.
Man U wanadaiwa kuwinda saini ya dogo huyo mwenye miaka 20, lakini Liverpool wametoa nje wakidai hawamuuzi.
Mazungumzo ya usajili Manchester United
Reviewed by Steve
on
Friday, May 22, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, May 22, 2015
Rating:
