Propellerads

Ujio wa Mustafi utamweka Ozil klabuni kwa muda mrefu



Imeripotiwa sasa Arsenal wanaweza kua na uhakika kwamba ujio wa Shkodran Mustafi
ndani ya Emirates utamweka Mesut Ozil kuwepo kwa muda mrefu zaidi.

Ozil kwa sasa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa lakini watendaji wa Gunners wanadaiwa kua tayari kwa maongezi katika wiki zijazo.

Kwa mujibu wa The Mirror kiungo huyo ambaye alijiunga na Arsenal miaka mitatu iliyopita, alisita kumwaga wino mpaka atakapoona jinsi upepo wa usajili utakavyokua katika klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

Inasemekana kwamba kusajiliwa kwa mjerumani mwenzake Mustafi ambaye ni rafiki wa karibu wa Ozil kunaweza kumshawishi kukaa kwa muda mrefu zaidi.

Ozil tayari amejadiliana na washauri wake kuhusu mkataba mpya ambao utakua na thamani ya pauni 200 000 kwa wiki.
Ujio wa Mustafi utamweka Ozil klabuni kwa muda mrefu Ujio wa Mustafi utamweka Ozil klabuni kwa muda mrefu Reviewed by Steve on Friday, September 02, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.