Koulibaly afafanua kwanini alikataa kutua Chelsea
Beki wa kati wa Napoli, Kalidou Koulibaly amedai kua aliamua kuwatosa Chelsea
katika kipindi cha dirisha la usajili kwa sababu anajisikia vizuri na klabu yake ya sasa.
Ilikua wazi kwamba Chelsea walikua wanajiandaa kuvunja rekodi yao ya usajili kumnasa beki huyo lakini ghafla wakabidilisha mpango wao na kumchukua tena aliyekua beki wao Davi Luiz.
Koulibaly, ambaye ni Msenegal amedokeza kwamba ilikua ni maamuzi yake mwenyewe kuitosa ofa kutoka Chelsea kwa sababu alitaka kuendelea kuwepo klabuni Naples.
"Niliamua kukaa kwa sababu ninajisikia vizuri na hii timu" aliiambia Il Mattino.
Koulibaly afafanua kwanini alikataa kutua Chelsea
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 03, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 03, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment