Kuhusu usajili wa Mourinho, Scholes ana mtazamo huu
Paul Scholes amedai kua usajili wa nguvu alioufanya meneja wa Manchester United, Jose Mourinho
umewainua kwa kiasi kikubwa Red Devils.
Mabingwa hao mara 20 wa EPL wamenunua wachezaji wanne msimu huu wa usajili, Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na Paul Pogba wakicheza michezo mitatu na rekodi ya asilimia 100 ya ushindi.
Scholes ameiambia Sky Sports News "Ubora wa wachezaji ambao amewaleta, ni tofauti kubwa.
"Hata wachezaji wameanza msimu vizuri. Kuna ujasiri fulani umeletwa kikosini. Inakuinua sana ukisajili wachezaji wakubwa kama Pogba na Ibra."
Kuhusu usajili wa Mourinho, Scholes ana mtazamo huu
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 03, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 03, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment