Mourinho hakutaka Schneiderlin kuchukuliwa na klabu hii, kisa!?
Siku ya kufungwa dirisha la usajili kocha Jose Mourinho hakuonekana kua bize sana,lakini
ripoti zimedai kua alikwamisha uhamisho wa mchezaji wake mmoja kwenda kwa wapinzani wao ndani ya Premier League.
Kocha huyo mreno alikamilisha usajili wake kwa asilimia kubwa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, huku akimuuza James Weir pekee kwenda Hul City.
Hata hivyo ripoti mpya zinadai bosi huyo alikwamisha uhamisho wa nyota mfaransa Morgan Schneiderlin.
Nyota huyo amecheza dakika tano pekee kwa Red Devils katika michezo mitatu ya kwanza msimu huu huku akionekana kupata ushindani kutoka kwa Paul Pogba, Marouane Fellaini, Michael Carrick na Ander Herrera kupata namba katika kiungo wa kati.
Tottenham walifanya jaribio la mwishoni kumnasa Schneiderlin lakini Mourinho alikwamisha, hii ni kwa mujibu wa Daily Mail.
Inadaiwa bosi huyo wa United hataki kupoteza wachezaji wake kutokana na sababu kwamba klabu itacheza mashindano manne tofauti msimu huu kwa hiyo kubadilishana itakua muhimu.
Mourinho hakutaka Schneiderlin kuchukuliwa na klabu hii, kisa!?
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 01, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 01, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment