Propellerads

Granit Xhaka na uhusiano wake na Wenger



Granit Xhaka amefichua kwamba alifanya maongezi mara mbili au tatu na
Arsene Wenger na kudai kua kocha huyo ndiye sababu kubwa ya kujiunga Arsenal.

Gunners walimsajili Mswizi huyo kutoka Borussia Monchengladbach mapema kipindi cha usajili kwa pauni mil 30.

Pamoja na kukaa muda mfupi na Wenger, Xhaka amedai kua anampa heshima kubwa mno bosi wake.

"[Wenger] sio kocha utakayeongea nae kila siku," aliiambia Appenzeller Zeitung. "Wenger amezungumza na mimi mara mbili au tatu. Aliniambia alivutiwa jinsi ninavofanya mazoezi na pia nilivyo na nidhamu.

"Ni mtu mkubwa, ukimtazama unajua 'wow, huyu mtu amefanikiwa na ana uzoefu sana'. Heshima kwake ni kubwa sana."
Granit Xhaka na uhusiano wake na Wenger Granit Xhaka na uhusiano wake na Wenger Reviewed by Steve on Sunday, September 04, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.