Baada ya kutolewa kikosi cha klabu bingwa, wakala wa Yaya Toure azungumza
Yaya Toure ametendewa ndivyo sivyo baada ya kutowekwa kwenye kikosi kwenye
kikosi kitachoshiriki Champions League.
Bosi wa Man City, Pep Guardiola alifanya maamuzi hayo Ijumaa iliyopita bila kumpa taarifa yoyote raia huyo wa Ivory Coast kwamba hatakuwemo kwenye kikosi hicho.
Wakala , Dimitri Seluk amefunguka katika gazeti la Sunday Mirror Sport Toure atabaki kutumikia mwaka wake wa mwisho Etihad pamoja na kutolewa.
Lakini Seluk anaamini Guardiola atamwomba msamaha kiungo huyo kama akishindwa kuchukua ubingwa wa Ulaya.
"Ni maamuzi ya Pep, tunayaheshimu," alisema Seluk.
"Kama akishinda klabu bingwa msimu huu na City nitasafiri mpaka England na nitazungumza katika televisheni kwamba Pep Guardiola ni kocha bora ulimwenguni.
"Lakini kama City wasiposhinda Champions League nadhani Pep atapata sababu ya kusema alikosea kutomtendea haki mchezaji mkubwa kama Yaya.
"Yaya ni mchezaji professional kwa hiyo atafanya kila anachoambiwa."
Baada ya kutolewa kikosi cha klabu bingwa, wakala wa Yaya Toure azungumza
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 04, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 04, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment