David Luiz atoa ya moyoni kilichomrejesha tena Chelsea
Nyota aliyesajiliwa na Chelsea kwa mara nyingine tena, David Luiz amefunguka
kuhusu uhamisho wake wa kurejea klabuni hapo na kwanini amerejea tena.
Luiz ambaye amejiunga tena na Chelsea baada ya kusajiliwa na Paris Saint-Germain kwa pauni mil 50 miaka miwili iliyopita amefichua kwamba ana furaha kurejea darajani na hakutaka kujiuliza kupoteza muda kuvaa uzi wa klabu hiyo kwa mara nyingine tena.
"Nina furaha kurejea Chelsea," alisema kama alivyonukuliwa na Daily Star.
"Tulikua na historia nzuri kipindi changu cha mwanzo klabuni hapa na ninataka kuisaidia timu na Antonio Conte kufikia mafanikio makubwa.
"Daima nilikua na uhusiano mzuri na mashabiki, na ninaangalia mbele kuvaa jezi ya blue nikiwa Stamford Bridge kwa mara nyingine tena."
David Luiz atoa ya moyoni kilichomrejesha tena Chelsea
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 01, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 01, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment