Baada ya tetesi za kutemwa Chelsea, huenda Fabregas akaelekea klabu kubwa ya Serie A
Imeripotiwa kua Chelsea wapo tayari kumruhusu kiungo Cesc Fabregas kujiunga
na Inter Milan, ikiwa ni jaribio la kumpata Marcelo Brozovic katika dili ambalo itakua ni kama kubadilishana.
Mhispani huyo jumapili hii alisisitiza kwamba bado yupo sana Chelsea, pamoja na uvumi kwamba kocha Antonio Conte amemfungulia mlango wa kutokea.
Kwa mujibu wa chapisho moja la kihispania, Gazzetta dello Sport, Chelsea wanataka kumnasa Brozovic na wanataka kumtumia Fabregas kama chambo katika kusaidia kufanikisha dili hilo.
Baada ya tetesi za kutemwa Chelsea, huenda Fabregas akaelekea klabu kubwa ya Serie A
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 30, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment