Propellerads

Arsenal wamekaribia kukamilisha dili la Mustafi



Arsenal wameripotiwa kua mwishoni kukamilisha uhamisho wa beki
wa kati wa Valencia, Shkodran Mustafi.

Gunners wamekua wakihusishwa na beki huyo kwa wiki kadhaa sasa huku Arsene Wenger akihangaika kuimarisha safu yake ya ulinzi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili jumatano ijayo.

Klabu hizo mbili zimekua zikipishana kuhusu swala la bei kwa mjerumani huyo, lakini BBC Sports wameripoti kua sasa Arsenal wamekubali matakwa ya Valencia ambapo watatoa pauni mil 35 zaidi.

Mustafi anatarajiwa kuchukua vipimo vya afya, lakini dili linaweza kua halijakamilika kwa muda kiasi cha kumwezesha kucheza mechi ya jumamosi ugenini dhidi ya Watford.


Arsenal wamekaribia kukamilisha dili la Mustafi Arsenal wamekaribia kukamilisha dili la Mustafi Reviewed by Steve on Friday, August 26, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.