Arsenal kumsajili fowadi kutoka Deportivo
Arsenal wamefanya makubaliano na klabu ya Deportivo La Coruna
kumsajili mshambuliaji Lucas Perez.
Inadaiwa kua Gunners wangeweza kukamilisha usajili wa Mhispania huyo leo, baada ya kuweka ofa ya pauni mil 17.1
Ghafla tetesi kutoka Hispania zikadai kua Deportivo wamelikataa dau hilo la Arsenal, lakini sasa BBC Sport wameripoti kua vilabu hivyo vimekubaliana dau hilo hilo la pauni mil 17.1
Arsenal kukamiisha dili la Mustafi
Lucas amekua akihusishwa na Everton, lakini Arsenal wameingilia dili na sasa wanaonekana kukaribia kukamilisha dili hilo.
Mshambuliaji huyo ambaye alimaliza msimu uliopita wa La Liga akiwa na magoli 17, anaweza akaungana na beki wa Valencia, Shkodran Mustafi baada ya Gunners kuripotiwa kufikia dili.
Arsenal kumsajili fowadi kutoka Deportivo
Reviewed by Steve
on
Friday, August 26, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, August 26, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment