Propellerads

Arsenal sasa macho yao kwa beki wa Monaco



Arsenal wameripotiwa kua na mpango wa kufanya uhamisho wa beki
kutoka AS Monaco, Marcel Tisserand wakiendelea na mpango wao wa kusaka beki mpya.

Bosi wa Gunners, Arsene Wenger hivi karibuni aliweka wazi kua anataka kuimarisha ulinzi kabla ya dirisha a usajili kufungwa kufuatia  Per Mertesacker na Gabriel Paulista kuandamwa na majeraha.

Shkodran Mustafi kutoka Valencia alikua anaonekana kama chaguo namba moja kwa Wenger, lakini swala la bei limeonekana kumshinda kwani kabu hiyo wanataka pauni mil 50.

Kwa mujibu wa The Sun Tisserand sasa ndiye chaguo la wakai hao wa kaskazini mwa London  japo wiki kadhaa zilizopita pia alihusishwa na Espanyo.

Tisserand anaweza kucheza beki ya kati na ya kulia, lakini anaonekana kukosa namba ya kudumu Monaco kwani alikua akitumika kwa mkopo ewns na pia Toulouse.
Arsenal sasa macho yao kwa beki wa Monaco Arsenal sasa macho yao kwa beki wa Monaco Reviewed by Steve on Wednesday, August 24, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.